Kwa kutumia tovuti ya FrajuuConnect, unakubaliana na masharti yafuatayo:
FrajuuConnect ni jukwaa la kuwezesha mawasiliano kati ya wauzaji/mawakala wa nyumba na wanunuzi/wapangaji. Hatuhusiki na maamuzi ya biashara kati ya pande hizi mbili.
Watumiaji wanawajibika kwa usahihi wa taarifa wanazoweka kwenye tangazo. FrajuuConnect haina dhamana juu ya uhalali wa taarifa hizo.
Hatuhusiki na malipo yoyote kati ya muuzaji na mnunuzi. Unashauriwa kuchukua tahadhari kabla ya kufanya malipo yoyote.
Unapojisajili kama ajenti au muuzaji, unapaswa kutoa taarifa sahihi. Akaunti itakayothibitika kuwa ya udanganyifu inaweza kufutwa bila taarifa.
Yaliyomo kwenye tovuti hii yanamilikiwa na FrajuuConnect isipokuwa yaliyowekwa na watumiaji. Hairuhusiwi kunakili au kutumia maudhui bila idhini.
Tunaweza kufanya mabadiliko ya masharti haya wakati wowote. Watumiaji wanashauriwa kuyapitia mara kwa mara.
Kwa maswali au malalamiko, wasiliana nasi kupitia barua pepe: info@frajuudigitals.com.
Tarehe ya Kuanza Kutumika: Mei 2025